Katiba ni moyo wa taifa: Samata

Posted: November 23, 2011 in Uncategorized
Tags:

Katika mdahalo ulioandaliwa Novemba 17/18 2011 na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ili kuadhumisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samata katika mdahalo alipokuwa akitoa mada kuhusu katiba alisema Katiba ni moyo wa taifa na mapatano yanayohusu namna nchi ikatavyoendeshwa, viongozi watakavyopatikana, watu watachaguliwa namna gani na nani atakayechagua kwa njia ipi. Kwa maana hiyo ili nchi na taifa iwe pahala pazuri ni lazima katiba yake ikidhi haja ya watu.
Samata alisisitiza kuwa kwa kuangalia katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kuna ubovu ambao sharti uondolwe kabla hatujaenda kule ambako wengine wamefika kwa kupigana ili kupata katiba mpya.
Ubovu wa Katiba ya Sasa ni Pamoja na;
Spika wa bunge bado anaweza kuwa mbunge. Kwa sababu sifa moja wapo ya kuwa Spika ni lazima awe na sifa ya kuwa mbunge.
Ibara ya 67(1) (b) lazima awe mtu ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa. tatizo la hili ni kuwa hawezi kusimamia maslahi ya taifa zaidi ataendelea kusimami na kutetea maslahi ya chama chake. Huu ni utaratibu uliotokana na dhana ile ya chama kimoja na kuondoa uwezekano wa mtu asiyemwaminifu kwa chama asiwe spika. Uchaguzi wa spika husimamiwa na tume ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi ambayo makamishiona huteuliwa na rais [ibara 74(1), (2)].
Kuonyesha kuwa tume si huru zaidi ni pale ambapo rais anaweza kumwondoa kamishiona [ibara 74(5)]
Tume ikishatangaza matokeo ya uchaguzi hakuna chombo kinachoruhusiwa kuhoji maamuzi yake [ ibara 74 (12)]. Tume huru ya uchaguzi ni idara. Kwanini iwe idara kwanini isiwe chombo huru? Hakuna mahakama hata mmoja itakayohoji maamuzi ya tume ya uchaguzi, kwa maana hiyo chama kinaweza ku-armtwist tume na ikawa ndivyo. Hakuna chombo itakayohoji uchaguzi wa rais ikishatangazwa. Hili yaweza kuwa chanzo cha wagombea wengine kutotendewa haki.
Mfano katiba ya Jamhuri ya Afrika Kusini [ibara 52(ii)] inasema kuwa uchaguzi wa spika lazima isimamiwe na jaji mkuu ama na mtu ambaye yeye atamteua suala ambalo litawapa haki wagombea wote wa nafasi ya uspika.

Mgombea binafsi Mfumo wa sasa haumpi nafasi mgombea binafsi, mwaka wa 1995 mahakama ilitoa hukumu kuwa mgombea binafsi anaruhusiwa kulingana na haki za binadamu kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ibara 20, 21). Lakini bungeni lilipinga maamuzi hayo na kuzuia ugombea binafsi na hii ilidhihirisha dhana ya chama kushika hatamu.

Inaruhusu imla wa wengi kwa kuwa uwingi ndiyo huamua nani ana haki ya jambo Fulani si haki.

Madaraka na mamlaka serikali hutokana na wananchi lakini sehemu ambapo mamlaka na madaraka ya bunge na mahakama yamebainishwa kuwa yanatokana na nani [ibara 8(1)]

Kura ya Maamuzi – referendum hakuna sehemu inayosema wananchi wana nafasi ya kuridhia mabadiliko. Kwa maana hiyo kuna uwezekano wa bunge kuamua jambo lolote bila hata wananchi kuridhia. Hata mabadiliko ya katiba yatafanywa na bila hata ridhaa ya wananchi. Mfano bunge linaweza kuamua tu kuwa Tanzania ni sehemu ya uganda na ikawa sawa.

Uteuzi wa Jaji Mkuu na Majaji Rais ana mamlaka makubwa ya kuteua majaji lakini bila maelekezo ya namna ya kuteua jaji. Vilevile anaweza kuamua kumvua ujaji mkuu Yule ambaye yeye amemteua, ni huku ni kuingilia uhuru wa mahakama kama chombo huru au mhimili wa dola.

Jaji Samata vile alisema katika mambo ambayo inatakiwa kila mtanzania ajiulize wakati wa mjadala wa katiba mpya ni pamoja na haya;
• Muundo wa muungano tunahitaji muundo huu uendelee au tuwe na serikali ya shirikisho/serikali tatu; Jamhuri Muungano wa Tanzania
[Tanzania Bara (Tanganyika)
Tanzania Visiwani (Zanzibar)]?
• Nafasi ya rais wa Zanzibar aendelee kama waziri asiyekuwa na wizara ama tutaiwekaje kwenye katiba mpya?
• Mfumo wa uchaguzi ambapo mwenye kura nyingi katika wote wanaogombea bila kuzingatia asilimia yaani Simple Majority-First Past The Post au Majority Votes yaani asilimia 50+ ya kura zote urais au tutaweka nafasi sawa na idadi za kura zilizopigwa Proportional Representation kama ya Jamhuri ya Afrika Kusini?
• Mgombea binafsi kwa sababu tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi na katiba hata ya sasa inatambua haki ya kupiga kura na kupigiwa kura tutaendelea kuwalimisha watu wawe wanyenyekevu kwa vyama vyao au kwa kuangalia uwezo wao.
• Mawaziri wawe wabunge au ama wawe mawaziri na wawajibishwe na bunge vilevile watumikie taifa bila kuwa na mgongano wa maslahi kati ya kuitetea serikali na kuwakilisha wananchi wake.
• Idadi ya mawaziri ijulikane kikatiba ama tutamwachia rais na uteuzi wao ufanyike na jopo maalum wakiwafanyia usaili na kuchunguza mienendo yao ya kimaisha yao yaani vetting; wanalipa kodi, wamewahi kudhulumu nk
• Kupinga au kutopinga uchaguzi wa rais ili kutenda haki kwa wasiyokuwa na hakika na imani na tume ama matokeo yalotangazwa.
• Wakuu wa wilaya wawepo au wasiwepo
• Sifa za spika ziwe zipi
• Uteuzi wa makamishioni wa tume ya uchaguzi uwe wa namna gani na nani ahusike nao
• Ukubwa wa bunge letu, ama tuanzishe baraza la juu –seneti na wawe na sifa zipi
• Rais awajibikaje na namna gani na kwa kueleza mafanikio kwa kipindi Fulani
• Je, bunge liendelee na utaratibu wa kubadilisha vifungu vya katiba bila wananchi kuridhia-referendum
• Adhabu ya kifo iendelee na kwa makosa yapi, na kama inafutwa ama itumike vipi ili watu wasije nyongwa hata walionewa.
• Mahakama ya kadhi, zianzishwe Tanzania bara, mfumo gani, ziwe na uhusiano gani na mfumo wa mahakama za kawaida.
• Mahakama ya katiba
• Mshindi wa urais apate 50+ au tuendelee na mfumo wa sasa
• Vipindi vya rais viwili tu na baada ya kukaa nje ya madaraka aombe tena kuwa rais kama Urusi?
• Misingi mikuu ya utawala
• Viti maalum vigezo vipi vitumike
• Wabunge wa kuteuliwa ni wakina nani na wanalenga kuwakilisha akina nani
• Uraia wa nchi mbili
• Wafungwa na mahabusu waruhusiwe kupiga kura
• Meya achaguliwe
• Itikadi ya dola
• Kudumisha misingi-dola na misingi
• Haki za wanawake, watoto na wazee na walemavu wa viungo vya mwili
• Ardhi ipewe kipengele ama sura maalum katika katiba ya nchi
• Uhuru wa maoni na vyombo vya habari
• Tunu za taifa zibainishwe na uzalendo ujengwe kwa njia ya katiba.

Katika haya maswali, jiulize wewe ungependa swali lipi lipatiwe ufumbuzi kwa haraka?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s