Utaifa Wetu Hatarini!

Posted: March 31, 2012 in Development, Nationalism, Politics, Tanzania
Tags: , , ,

Utaifa ni jambo ambalo ujenzi wake huchua muda sana kutekeleza. Kama kujenga nyumba, watu wengine hufa bila kujenga nyumba, wengine hufa kwenye nyumba za kupanga na wengine hubaki kulalamikia watu wa nyumbani kwao kuwa ni wachawi, washirikina na hawapendi maendeleo hivyo huogopa kujenga.

Ukweli ni kuwa ni ugumu wa kujenga ndiyo huleta ukwepaji wa wajibu wa kujenga nyumba wakitafuta visingizio. Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge Kijana wa Mtera Livingstone Lusinde (Sikiliza Matusi yake Hapa) (CCM) anayejulikana kwa jina la utani kama kibajaji, ameporomosha matusi na ambayo kama taasisi zetu zingekuwa zinafanya kazi zake basi zisingechelea kumfungulia mashtaka ya kuchafua majina ya watu kwa kutumia jukwa la siasa ambapo si kisingizio cha kuruhusu hisia na ujinga, upumbavu na siasa za kugawa watu.

Matusi hayo na maneno hayo yasiyo na staha aliyazungumza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki katika eneo la Usa River. Kumeibuka kundi la wanasiasa vijana ambao hawatambui juhudi kubwa na nguvu nyingi nyingi zilizotumika kujenga UTAIFA huo ambao unawaruhusu kutoa maneno yasiyo ya staha na mara nyingine maneno ya kugawa waTanzania kwa mtazamo wao kisiasa, kimaeneo na dini.

Mwalimu Nyerere alitumia muda mwingi kujenga utaifa huo hata kuna wakati ugumu kutoka kwa wananchi, wanasiasa wenziye, viongozi wa dini lakini mwishowe alifanikiwa kuleta umoja huo uliotambuliko hata nje ya nchi.

Kuna hatari na kule tunakoelekea ni kubaya zaidi ya tuwezavyo kufikiri. Tanzania ni kubwa zaidi ya wabunge, wanasiasa, wabinafsi, wanaharakati, CCM, CHADEMA, CUF na ADC na viongozi wa kidini, hivyo anayetaka kuturudisha kwenye enzi za unazi wa kijerumani na hata enzi za fikra za mwenyekiti zidumu hata kama si sahihi, watafakari vyema malengo yao kwa taifa hili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s